USIJILAZIMISHE/USIMLAZIMISHE MTU KUFANYA JAMBO/KAZI ASIYOIPENDA KWASABABU ZA MSIMU

Sunday, January 6, 2013

Usifanye/usimlazimishe mtu kufanya jambo/kazi kwa sababu za msimu, bali fanya jambo hilo kwasababu moyoni mwako umedhamiria na unapenda kulifanya.

Watu wengi sana wanafanya jambo/kazi si kwasababu wanapenda kufanya bali wanatamani kufanya kutokana na sababu za msimu ambapo siku sababu hizi zikiisha na wao wanaacha. Na wengine wanadiriki kuwalazimisha watoto wao kusomea courses ambazo watoto hawa hawazipendi kisa wazazi wanazipenda na walikua wanazifanya... matokeo yake tunakua na wataalam ambao hawana bidii katika kazi zao na wengine imewapelekea kubadilisha fani ukubwani, ambapo kama wazazi wangejua watoto wao wanapenda kufanya nini tangu utotoni, wangezipa courses hizo kipaumbele alafu hizo nyingine zingefuata baadae. Na ndio maana kuna maendeleo makubwa sana pale mtu anapofanya kazi ambayo anaipenda, tofauti na yule anayefanya kazi asiyoipenda.

- Mfano, usiwe mwanasiasa kwasababu tu unatafuta umaarufu na kuheshimiwa au umeambiwa kuna kula, siku kula itakapoisha na siasa utatupilia mbali....

- Usiwe mtunga mashairi kwasababu tu uko inlove, maana siku ukiumizwa na mashairi yataisha...

- Usiwe mhubiri kwasababu unapitia katika maisha magumu, maana siku ukipata utajiri na kuhubiri kutaisha...

- Usiimbe kwasababu ni fashion, kila mtu anaimba, siku fashion ikipita na kuimba kwako kutaisha..

- Usiwe mshauri kwasababu ulitendwa, siku maumivu yakiisha na ukampata umpendaye, utakua huna tena cha kushauri...

- Usifanye jambo eti kwasababu na wengine wanafanya, maana siku wakiacha kufanya nawe utaacha na kuona halina maana...

Na siku utakayoacha kufanya hayo, litawaathiri wengi hasa wale waliokuwa wanakutegemea katika hilo unalofanya. Fanya jambo kwasababu unapenda kutoka moyoni kulifanya, hata siku upate dhoruba hutatetereka, utafanya kwa bidii, bila kujilazimisha.
#Via Funguka@upendomashina. blogspot.com

0 comments:

Post a Comment