KILA SEKUNDE KATIKA MAISHA YAKO NI YA THAMANI SANA!

Friday, May 18, 2012

Angalia sana jinsi unavyotumia muda wako, kwani kila sekunde ikishapita haiwezi kujirudia tena milele. Jitahidi sana kutenda mambo mazuri, kubuni vitu mbalimbali na pia kuwa mfano wa kuigwa kwa wengine ili hata baadae ukiwa haupo, watakaokuwepo waweze kujivunia mambo yako mazuri uliyoyafanya.

Wapo watu wengi sana ambao walifanya mambo ambayo sio mazuri na wakajisahau kabisa wakidhani  kuwa muda umesimama kuwangoja, kilichowapata ni kwamba, walipokuja kushtuka wakaanza kujutia na kutamani kurudisha muda nyuma ili wajirekebishe kitu ambacho hakikuwezekana.

Pangilia muda wako vizuri, na utumie kila sekunde vizuri katika kujiletea maendeleo, kwani kuna msemo usemao "time is money"

Barikiwa!

0 comments:

Post a Comment