Funga mwaka yangu ni hii hapa: Acha kutamani kiti cha hukumu cha Mungu.

Friday, December 14, 2012

Namshukuru Mungu aliyeniwezesha kuiona siku ya leo, na ningependa tujifunze jambo hili.. watu wengi wamekuwa mstari wa mbele kuhukumu wengine na kuwanyooshe vidole, wakasahau Yesu aliposema katika Math. 7:1-5 Msihukumu, msije mkahukumiwa ninyi. Kwakuwa hukumu ile mhukumuyo, ndiyo mtakayo hukumiwa; na kipimo kile mpimiacho, ndicho mtakachopimiwa.Basu, mbona wakitazama kibanzi kilicho ndani ya jicho la ndugu yako, na boriti iliyo ndani ya jicho lako huiangalii? Au utamwambiaje nduguyo, niache nikitoe kibanzi katika jicho lako; kumbe mna boriti ndani ya jicho lako mwenyewe? Mnafiki wewe, itoe kwanza ile boriti katika jicho lako mwenyewe; ndipo utakapoona vyema kukitoa kile kibanzi katika jicho la ndugu yako."

Hili neno linatufundisha kwamba tuache tabia ya kuhukumu wengine, tusipende kuhukumu kwa kazi ya kuhukumu ni ya Mungu pekee. Hapa elewa sitetei dhambi, kama mtu amefanya dhambi muonye na kumfundisha njia sahihi na sio kumhukumu na kumnyooshea vidole. Utamkuta mtu mwingine amemwona mwenzake kakosea badala ya kumuonya anakuwa mstari wa mbele kutangaza kila mahali kosa la yule mtu, wakati yawezekana kosa hilohilo huyu mtu analifanya kwa siri.

Nataka nikupe mfano ili ujue unavyomhukumu mwingine na wewe yawezekana uko kwenye mstari huohuo sema hujui. Hata Yesu aliposema haya maneno aliona mbali sana. Angalia hapa dhambi zinavyofanana alafu ndo uwe wa kwanza kusogea karibu na kiti cha hukumu uhukumu wengine. Aliyezini na aliyemtazama mwanamke kwa kumtamani au aliyemtamani mwanaume wote wamezini, aliyechukua cream akajichubua na aliyeenda photo studio na kupiga picha alafu akaomba waedit hiyo picha na kuondoa vidoa doa vya asili vilivyoko kwenye picha halisi au chunusi, wote wamekosoa uumbaji wa Mungu, aliyechukua bastola akamwua mtu na aliyetamka kwa maneno au aliyetumia maneno kuumiza wengine wote ni wauwaji, unatekata nywele zako wakati umepewa zirefuke na anayesukia weaving wote mmekosoa uumbaji wa Mungu, kusingizia, kusema uongo, wizi, ufisadi, dharau, na mengine kama hayo yote ni dhambi, aliyelewa mvinyo na aliye kula kwa ulafi ndo wale wale.. sasa huwezi mhukumu mtu yeyote, wala hakuna anayestahili kusongea karibu na kiti cha hukumu cha Mungu, kama mtu amekosea muombee rehema kwa Mungu na umuonye. Kumbuka hakuna dhambi ndogo wala kubwa, zote ni dhambi,, huwezi sema uwongo alafu umhukumu aliyeiba, huwezi msingizia mtu alafu umhukumu aliyeua..

Nakutakia kila laheri katika maandalizi ya Christmas na mwaka mpya, tukutane mwaka ujao katika blog hii kwaajili ya kujifunza mengi ya kimwili na kiroho pia, pia utakuwa unapata habari mbalimbali zinazohusu urembo na style mbalimbali za mavazi na nywele.

2 comments:

Post a Comment